Subscribe to this channel

You can subscribe to new audio episodes published on this channel. You can follow updates using the channel's RSS feed, or via other audio platforms you may already be using.

RSS Feed

You can use any RSS feed reader to follow updates, even your browser. We recommend using an application dedicated to listening podcasts for the best experience. iOS users can look at Overcast or Castro. Pocket Casts is also very popular and has both iOS and Android versions. Add the above link to the application to follow this podcast channel.

Signup to iono.fm

Sign up for a free iono.fm user account to start building your playlist of podcast channels. You'll be able to build a personalised RSS feed you can follow or listen with our web player.
04
MAY

KISWAHILI NEWS: TANZANIA YAAGIZA DAWA YA KUTIBU COVID19 KUTOKA MADAGASCAR

Rais wa Tanzania JOHN MAGUFULI amesema nchi yake itaagiza dawa za asili zinazodaiwa kutibu wagonjwa wenye virusi vya homa kali ya mapafu unaosababishwa na Covid- 19 kutoka nchini Madagascar.
Pia mbali ya kuagiza dawa hizo za asili,Rais huyo wa Tanzania ametilia mashaka majibu ya sampuli za vipimo vya Corona vinavyotolewa na maabara kuu ya taifa la nchi hiyo na kusema huenda baadhi ya wale wanaopimwa na kuambiwa wameambukizwa virusi vya Covid19 siyo kweli.
Mwandishi wetu Gabriel Zakaria ana maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam.
Kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa jana jumapili kijijini kwake Chato kaskazini magharibi mwa Tanzania inaifanya Tanzania kuwa katika orodha ya nchi chache Afrika yaliyoonyesha nia ya kuagiza dawa za asili kutoka Madagascar kutibu wagonjwa wenye virusi vya Corona.
Dawa hiyo kutoka Madagascar inayojulikana kama Covid-Organics (CVO) inadaiwa kutengenezwa kutokana na mmea unaojulikana kama Artemisia – chanzo cha viungo vinavyotumiwa kutengeneza dawa ya kutibu malaria.
Mbali na kuagiza dawa za kutibu wagonjwa wa Corona,Rais Magufuli ameonyesha wasiwasi wa majibu ya sampuli za maambukizi ya Covid-19 yanayotolewa na maabara kuu ya Tanzania,na kusema huenda kuna hujuma ndani yake.
Mashaka ya Rais Magufuli kuhusu usahihi wa majibu ya sampuli za maabara,unamuibua Rais wa Chama cha wataalam wa sayansi ya maabara ya afya nchini Tanzania Mnung’a ambaye hapa anakosa uvumilivu na kueleza haya.
Lakini tofauti na viongozi wa mataifa jirani ya Uganda na Kenya, Dkt Magufuli ameshikilia msimamo wake kuwa kamwe hatatoa amri ya kudhibiti shughuli za kawaida katika miji mikuu kama vile Dar es Salaam na Dodoma.
Aidha, ametangaza kuwa siku chache zijazo anafikiria kuruhusu kurejelewa kwa ligi kuu ya kandanda nchini Tanzania akisema “imebainika wazi kuwa wanaspoti hawaambukizwi virusi vya corona.
Kwa sasa Tanzania ina idadi ya wagonjwa 480 walioambukizwa virusi vya Covid-19 na kufanya kuwa ya kwanza katika ukanda wa nchi 6 za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa na

992 episodes

« Back 1—12 More »