#1  Nitafanya nini? - Episode 1

Katika mchezo wa Kizazi njia panda, tunaingia kwenye awamu mpya ya mfululizo wa vipindi vipya vya Noa bongo - Jenga maisha yako. Hivi ni vipindi vya kuelimisha vinavyotayarishwa na Deutsche Welle kwa ajili ya vijana wa Afrika. Sikiliza awamu ya pili ili kukutana tena na nyota wa mchezo huu wa redio, Mercy, Dan, Niki na Trudy, huku ukifuatilia hadithi yao katika michezo ya redio kila wiki. Kwa mara ya kwanza utapata fursa pia ya kuwaona baadhi yao katika mkanda mpya wa vidio kila baada ya wiki moja.